3: NJIA SAHIHI YA KUWALEA WATOTO

 السلام عليكم ورحمة الله وبركاته .💖 


الحمد لله رب العالمين والصلاة والسلام على أشرف الأنبياء والمرسلين وبعد: 


USAWA BAINA YA WATOTO KATIKA UISLAAM. 👨‍👩‍👧‍👦

               (*Malezi sahihi kwa watoto*)



Uislaam umejaalia kuwa watoto ni viburudisho vya nyoyo. Ili hili liweze kutimia ni lazima tuoneshe kwa vitendo, nayo hutimia katika kuwafanyia usawa watoto katika nyumba yako. 🏡🏠


 ⏳ Usawa sio katika kula🥖🥝 na kulala tu, bali hata kuwabusu na kucheza nao.  

Usije ukambusu mtoto mmoja ukamuacha wa pili, hii inaweza kuleta athari katika nafsi ya mtoto na kupelekea kujenga chuki na uadui baina yao wenyewe (watoto ) au baina yao na wazazi.


Na kuto kufanya uadilifu baiba ya watoto wa jinsia moja au jinsia tofauti kunapelekea kukiuka mafundisho na mwenendo wa kiislaam.  

Kwani inaelezwa kuwa mtume( rehma na amani ziwe juu yake ) alimkuta baba mwenye watoto wawili akimbusu mmoja na kumuacha wa pili, mtume alimuuliza jee huwezi kuwafanyia usawa??.


Tunaona uzito wa uadilifu kwa watoto ikiwa kwenye kubusu tu basi mtume amekemea. 


Vile vile tuelewe kuwa uislaam hautofautishi baina ya mtoto wa kiume na wa kike wote ni sawa, na kama tunavo jua kuwa zama za ujahili (yaani kabla ya kupewa utume mtume s.w.s) walikuwa wakizika watoto wa kike na kuacha wa kiume kwakuwa waliona mtoto wa kike ni aibu, Kwa hiyo mtume( صلى الله عليه وسلم) aliwapa daraja na cheo watoto wa kike ili wasiendelee kudharaulika na kuonekana ni kitu cha aibu.  


Na daima mtume aliusia watendewe wema watoto wa kike, kwasababu aliona wazazi wali mili (kuelemea) zaidi kwa watoto wao wa kiume. 


💫💫💫💫💫💫💫


Wanatakiwa wazazi kuwa makini katika malezi yao juu ya watoto wao na wajitahid kua wadilifu baina ya watoto wao kwani kuto kufanya hivyo kutapelekea kukimbia mapenz na amani katika majumba na familia. 

Na kwa kumalizia mola wetu ana sema  

 ( ٱعۡدِلُوا۟ هُوَ أَقۡرَبُ لِلتَّقۡوَىٰۖ)

Fanyeni uadilifu. Hivyo ndio kuwa karibu mno na uchamngu.

[سورة المائدة 8]  suratul maaida aya ya 8.


IMEANDALIWA NA: 💖AL-GHAITHIY 💖

                         ☺️الغيثي😊   


🦋 والسلام عليكم ورحمة الله وبركاته . 🦋

تعليقات

المشاركات الشائعة من هذه المدونة

4: MAONI YA UWISLAMU JUU YA MALEZI YA WATOTO

D:2 PENDO LA WAZAZI KWA WATOTO WAO. 👨‍👩‍👧‍👦