المشاركات

عرض المشاركات من أغسطس, ٢٠٢٠

D:2 PENDO LA WAZAZI KWA WATOTO WAO. 👨‍👩‍👧‍👦

       السلام عليكم ورحمة الله وبركاته  Assallamu alaykum warahmatu llah wabarakaatuh. الحمد لله رب العالمين والصلاة والسلام على أشرف الأنبياء والمرسلين وبعد: PENDO LA WAZAZI KWA WATOTO WAO. 👨‍👩‍👧‍👦 Mtoto ni matokeo ya kimaumbile yenye kupatikana kutokana na uhusiyano imara wa wazazi. Uhusiano wa wazazi kwa watoto ni miongoni mwa uhusiano ulio imara na wenye daraja ya juu zaidi kuliko uhusiano wowote ule mwengine usiyo kuwa huwo. 😊 Amesama allah subhanah wataala katika sura ya 30 (suuratu a ruum)  ( سورة الروم aya ya 21)  (وَمِنۡ ءَایَـٰتِهِۦۤ أَنۡ خَلَقَ لَكُم مِّنۡ أَنفُسِكُمۡ أَزۡوَ ٰ⁠جࣰا لِّتَسۡكُنُوۤا۟ إِلَیۡهَا وَجَعَلَ بَیۡنَكُم مَّوَدَّةࣰ وَرَحۡمَةًۚ إِنَّ فِی ذَ ٰ⁠لِكَ لَـَٔایَـٰتࣲ لِّقَوۡمࣲ یَتَفَكَّرُونَ)  Na katika ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao, Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu, Hakika katika haya bila ya shaka zipo ishara kwa watu wanao fikiri. Katika tafsir ya (qurtubi) kasema, amesema ibnu abbas n