المشاركات

4: MAONI YA UWISLAMU JUU YA MALEZI YA WATOTO

                           بسم لله الرحمن الرحيم            السلام عليكم ورحمة الله و بركاته🤝🏻   الحمد لله رب العالمين، والصلاة والسلام على رسول الله   محمد صلى الله عليه وسلم  :أما بعد  MAONI YA UISLAAMU JUU YA MALEZI YA WATOTO.  Watoto ni maua yanayo chanua na kunukia katika maisha yetu, vile vile ni nyota inayo nģara katika mustaqbali wetu (maisha yajayo).  Watoto ndio wenye jukumu la kudumisha historia ya mataifa yao na wao wanawajibu wa kutumia nguvu zao katika kulinda nchi na mataifa yao. Na kwasababu hiyo, ndipo uislaamu umehimiza sana umuhimu wa malezi ya mtoto. Kwani mtume s.w.s amesema  ( كلكم راع وكلكم مسئول عن رعية والرجل راع في أهله ... )  Maana ya *Hadidhi* nyote ni watu wenye kuchunga na kila mmoja ataulizwa juu ya anacho kichunga na mwana mme ni mchungaji juu ya watu wake na ataulizwa juu ya watu wake...  QUR'AN ina maagizo na masharti katika maisha ya mtoto pia kumuongoza na kumpangia utaratibu katika maisha yake. Kwani mtume wetu ame ashiriya kuhusu nid

3: NJIA SAHIHI YA KUWALEA WATOTO

 السلام عليكم ورحمة الله وبركاته .💖  الحمد لله رب العالمين والصلاة والسلام على أشرف الأنبياء والمرسلين وبعد:  USAWA BAINA YA WATOTO KATIKA UISLAAM. 👨‍👩‍👧‍👦                (*Malezi sahihi kwa watoto*) Uislaam umejaalia kuwa watoto ni viburudisho vya nyoyo. Ili hili liweze kutimia ni lazima tuoneshe kwa vitendo, nayo hutimia katika kuwafanyia usawa watoto katika nyumba yako. 🏡🏠  ⏳ Usawa sio katika kula🥖🥝 na kulala tu, bali hata kuwabusu na kucheza nao.   Usije ukambusu mtoto mmoja ukamuacha wa pili, hii inaweza kuleta athari katika nafsi ya mtoto na kupelekea kujenga chuki na uadui baina yao wenyewe (watoto ) au baina yao na wazazi. Na kuto kufanya uadilifu baiba ya watoto wa jinsia moja au jinsia tofauti kunapelekea kukiuka mafundisho na mwenendo wa kiislaam.   Kwani inaelezwa kuwa mtume( rehma na amani ziwe juu yake ) alimkuta baba mwenye watoto wawili akimbusu mmoja na kumuacha wa pili, mtume alimuuliza jee huwezi kuwafanyia usawa??. Tunaona uzito w

D:2 PENDO LA WAZAZI KWA WATOTO WAO. 👨‍👩‍👧‍👦

       السلام عليكم ورحمة الله وبركاته  Assallamu alaykum warahmatu llah wabarakaatuh. الحمد لله رب العالمين والصلاة والسلام على أشرف الأنبياء والمرسلين وبعد: PENDO LA WAZAZI KWA WATOTO WAO. 👨‍👩‍👧‍👦 Mtoto ni matokeo ya kimaumbile yenye kupatikana kutokana na uhusiyano imara wa wazazi. Uhusiano wa wazazi kwa watoto ni miongoni mwa uhusiano ulio imara na wenye daraja ya juu zaidi kuliko uhusiano wowote ule mwengine usiyo kuwa huwo. 😊 Amesama allah subhanah wataala katika sura ya 30 (suuratu a ruum)  ( سورة الروم aya ya 21)  (وَمِنۡ ءَایَـٰتِهِۦۤ أَنۡ خَلَقَ لَكُم مِّنۡ أَنفُسِكُمۡ أَزۡوَ ٰ⁠جࣰا لِّتَسۡكُنُوۤا۟ إِلَیۡهَا وَجَعَلَ بَیۡنَكُم مَّوَدَّةࣰ وَرَحۡمَةًۚ إِنَّ فِی ذَ ٰ⁠لِكَ لَـَٔایَـٰتࣲ لِّقَوۡمࣲ یَتَفَكَّرُونَ)  Na katika ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao, Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu, Hakika katika haya bila ya shaka zipo ishara kwa watu wanao fikiri. Katika tafsir ya (qurtubi) kasema, amesema ibnu abbas n

UMUHIMU WA MTOTO KATIKA UWISLAM KABLA YA KUZALIWA.

                       بسم لله الرحمن الر حيم                   السلام عليكم ورحمة الله وبركاته  Ndugu zangu katika iman leo tutaangalia  ✨ UMUHIMU WA MTOTO KATIKA UISLAAM KABLA YA KUZALIWA .  ▫Uislaam umetilia maanani kuhusu malezi ya mtoto kabla hajaanza kupata umbo tumboni. Nandio maana mtume (صلى الله عليه وسلم) amesema: "jitahidi upate(mke) mwenye kushikamana na dini, basi furaha zote ni zako" . Uzuri na utajiri si sifa pekee za kutosha kuchaguwa mke sambamba na sifa hizo mwanamke anatakiwa awe na sifa ya uchamungu, kwani watoto wake ndio warithi wa tabia zake.   ▫Vile vile mtume amemuelekeza yule alie tayari kuolewa amkubalie yule mwenye uchamungu na tabia za kidini. Mtume (صلى الله عليه وسلم) amesema: "atakapo kujieni yule mulie mridhia dini yake na akhlaq (tabiya) zake basi muozesheni ..."   ▫Kwavile uislaam umehimiza kumchagulia  mtoto mama mwema kabla kuja duniani mtoto huyo ndomana mtume ameonya kuoana na ndugu wa karibu ili watoto wasizaliwe madhaif