المشاركات

عرض المشاركات من سبتمبر, ٢٠٢٠

3: NJIA SAHIHI YA KUWALEA WATOTO

 السلام عليكم ورحمة الله وبركاته .💖  الحمد لله رب العالمين والصلاة والسلام على أشرف الأنبياء والمرسلين وبعد:  USAWA BAINA YA WATOTO KATIKA UISLAAM. 👨‍👩‍👧‍👦                (*Malezi sahihi kwa watoto*) Uislaam umejaalia kuwa watoto ni viburudisho vya nyoyo. Ili hili liweze kutimia ni lazima tuoneshe kwa vitendo, nayo hutimia katika kuwafanyia usawa watoto katika nyumba yako. 🏡🏠  ⏳ Usawa sio katika kula🥖🥝 na kulala tu, bali hata kuwabusu na kucheza nao.   Usije ukambusu mtoto mmoja ukamuacha wa pili, hii inaweza kuleta athari katika nafsi ya mtoto na kupelekea kujenga chuki na uadui baina yao wenyewe (watoto ) au baina yao na wazazi. Na kuto kufanya uadilifu baiba ya watoto wa jinsia moja au jinsia tofauti kunapelekea kukiuka mafundisho na mwenendo wa kiislaam.   Kwani inaelezwa kuwa mtume( rehma na amani ziwe juu yake ) alimkuta baba mwenye watoto wawili akimbusu mmoja na kumuacha wa pili, mtume alimuuliza jee huwezi kuwafanyia usawa??. Tunaona uzito w