4: MAONI YA UWISLAMU JUU YA MALEZI YA WATOTO

                           بسم لله الرحمن الرحيم

           السلام عليكم ورحمة الله و بركاته🤝🏻 

 الحمد لله رب العالمين، والصلاة والسلام على رسول الله   محمد صلى الله عليه وسلم

 :أما بعد

 MAONI YA UISLAAMU JUU YA MALEZI YA WATOTO.

 Watoto ni maua yanayo chanua na kunukia katika maisha yetu, vile vile ni nyota inayo nģara katika mustaqbali wetu (maisha yajayo).

 Watoto ndio wenye jukumu la kudumisha historia ya mataifa yao na wao wanawajibu wa kutumia nguvu zao katika kulinda nchi na mataifa yao. Na kwasababu hiyo, ndipo uislaamu umehimiza sana umuhimu wa malezi ya mtoto. Kwani mtume s.w.s amesema 

( كلكم راع وكلكم مسئول عن رعية والرجل راع في أهله ... )

 Maana ya *Hadidhi* nyote ni watu wenye kuchunga na kila mmoja ataulizwa juu ya anacho kichunga na mwana mme ni mchungaji juu ya watu wake na ataulizwa juu ya watu wake... 

QUR'AN ina maagizo na masharti katika maisha ya mtoto pia kumuongoza na kumpangia utaratibu katika maisha yake. Kwani mtume wetu ame ashiriya kuhusu nidhamu juu ya mtoto kwa kusema

 (مروا أولادكم الصلاة وهم أبناء سبع) 

 Maana ya *Hadithi* waamuruni watoto wenu swala nao wakiwa watoto wa miaka saba. Yote ina onesha umuhimu wa nidhamu. 

Na msikiti ni sehemu kama shule kwa muumini. Wakati uwislamu unapo panga utaratibu katika maisha ya mtoto, familia na jamii zinazingatia kwamba pana uhusiano wa ndani baina yao unaoonyesha kwamba mabadiliko au uharibifu wowote ukitokea upande mmoja basi utawadhuru wote. 

 Kwahivyo fikra za uislaamu zimempangia muislaamu njia nzuri ya maisha ambayo msingi wake ni ushirikiano, huruma na imani, mwenyezi mungu ame sema

 ( وَتَعَاوَنُوا۟ عَلَى ٱلۡبِرِّ وَٱلتَّقۡوَىٰۖ وَلَا تَعَاوَنُوا۟ عَلَى ٱلۡإِثۡمِ وَٱلۡعُدۡوَ ٰ⁠نِۚ ) 

                             (سورة المائدة 2) 

 Maana ya *aya* (Na saidianeni katika wema na uchamngu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui.) 

 Tutapo ishi kwa ushirikiano, huruma na imani basi kwa uwezo wa Allah tutafanikiwa kujenga taifa lililo bora. Na ikiwa tutapuuza na kuacha misingi ambayo Allah katuekea bc tutaharibikiwa.

  😇😇 IMEANDALIWA NA : AL-GHAITHIY. 🦋

                              .والسلام علبكم

تعليقات

المشاركات الشائعة من هذه المدونة

D:2 PENDO LA WAZAZI KWA WATOTO WAO. 👨‍👩‍👧‍👦

3: NJIA SAHIHI YA KUWALEA WATOTO