D:2 PENDO LA WAZAZI KWA WATOTO WAO. 👨‍👩‍👧‍👦

       السلام عليكم ورحمة الله وبركاته

 Assallamu alaykum warahmatu llah wabarakaatuh.


الحمد لله رب العالمين والصلاة والسلام على أشرف الأنبياء والمرسلين وبعد:



PENDO LA WAZAZI KWA WATOTO WAO. 👨‍👩‍👧‍👦




Mtoto ni matokeo ya kimaumbile yenye kupatikana kutokana na uhusiyano imara wa wazazi. Uhusiano wa wazazi kwa watoto ni miongoni mwa uhusiano ulio imara na wenye daraja ya juu zaidi kuliko uhusiano wowote ule mwengine usiyo kuwa huwo. 😊

Amesama allah subhanah wataala katika sura ya 30 (suuratu a ruum)
 ( سورة الروم aya ya 21)

 (وَمِنۡ ءَایَـٰتِهِۦۤ أَنۡ خَلَقَ لَكُم مِّنۡ أَنفُسِكُمۡ أَزۡوَ ٰ⁠جࣰا لِّتَسۡكُنُوۤا۟ إِلَیۡهَا وَجَعَلَ بَیۡنَكُم مَّوَدَّةࣰ وَرَحۡمَةًۚ إِنَّ فِی ذَ ٰ⁠لِكَ لَـَٔایَـٰتࣲ لِّقَوۡمࣲ یَتَفَكَّرُونَ) 

Na katika ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao, Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu, Hakika katika haya bila ya shaka zipo ishara kwa watu wanao fikiri.


Katika tafsir ya (qurtubi) kasema, amesema ibnu abbas na mujahid, makusudiyo ya mawadda katika hiyo aya ni upendo, na makusudiyo ya rahma katika hiyo aya ni watoto.

Namaanisha baadhi ya wfasiri wameeleza kuwa penz na huruma vinamaana ya "mtoto". 


Allah amefanya kuwapenda watoto na kuwahurumia ni sehemu ya maumbile ya kiasili.

 Na yeye allah ndie alie zidhibiti hisia hizi ndani ya nyoyo za wzazi.

Na ndio maana allah alimuusia mtoto kumtendea wema mzazi wake ili kuzidi kufanya mapenzi ya mzazi yawe makubwa zaidi kwa mtoto.


Tuna paswa kufahamu yakwamba pendo la mzazi ni pendo la asili.🥰

 Tuwatunze wazazi wetu ili mapenzi yao juu yetu yapate kuzidi. 🥰




🦋IMEANDALIWA NA: AL-GHAITHIY الغيثي.

                

                       🦋والسلام عليكم 🦋.

تعليقات

  1. Lugha rahisi ni nzuri kutumika katika kufasiri au utohowaji wa misamiati katika lugha nyengine. Ili wasomaje waweze kufahamu zaid

    ردحذف

إرسال تعليق

المشاركات الشائعة من هذه المدونة

4: MAONI YA UWISLAMU JUU YA MALEZI YA WATOTO

3: NJIA SAHIHI YA KUWALEA WATOTO